ADA ZA UANACHA - 2007

Camillus Ahuya, IGA Country Representative - Kenya

IGA - Kiswahili

Karibu Katika Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi

Asante kwa kutumia muda wako kutembelea tovuti yetu. Mwaka 2006 kwa msaada wa wanachama zaidi ya 250 na washirika wengine kutoka nchi mbalimbali 61, Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi uliendelea kuhamasisha utafiti na maendeleo ya mbuzi duniani kote. Mwaka 2007 umoja huo unaadhimisha mwaka wa 25 tangu kuanzishwa kwake. Umoja unajivunia mafanikio uliyoyapata na ndani ya kipindi cha historia yake. Umoja unawategemea sana wanachama wake wenye ujuzi wa aina mbalimbali na uzoefu wa muda mrefu kama wewe kutimiza majukumu yao kwenye umoja huu, jamii zao, nchini mwao na duniani kwa ujumla.

Tutaendelea kupanuka na kuboresha juhudi zetu za awali. Jiunge leo na utasaidia kuhakikisha kuwa juhudi zetu zinaangaza umuhimu wa mbuzi katika kuboresha maisha ya watu duniani kote kwa miaka mingine 25 ijayo.

Hivi sasa tunajiandaa kwa Kongamano la tisa (9) la kimataifa kuhusu mbuzi ambalo litafanyika mjini Queretaro, Mexico, tarehe 31 agosti hadi tarehe 4 Septemba mwaka 2008, tunaamini kuwa unaweza kutusaidia kufanya Kongamano hili liwe na mafanikio makubwa. Moja ya malengo ya umoja wa wadau wa Mbuzi Kimataifa ni kuhakikisha kuwa wanataaluma mbalimbali vijana na hasa wanawake wanaopenda maswala ya utunzaji/uzalishaji na utafiti wa mbuzi wanashiriki katika Kongamano hili. Hivyo tunahitaji msaada wako ili kuweza kuwadhamini baadhi ya wanataaluma vijana ambao hawataweza kumudu gharama za kushiriki Kongamano hili. Wastani wa gharama zinazohitajika kudhamini ushiriki wa mwanataaluma mmoja kijana ni dola za Kimarekani elfu moja na mia tano ($ 1,500) ambazo zitatumika kwa kugharamia usafiri wa ndege, chakula na malazi.

Tafadhali saidia kudhamini wanataaluma vijana: Ili kujifunza zaidi bofya hapa.

Wenu
Chris Lu
Raisi wa Chama cha wadau wa mbuzi

Wasiliana nasi kwa njia zifuatazo:
International Goat Association
Aione: Christian DeVries
Director of Operations
1 World Avenue
Little Rock, Arkansas 72202 USA
Simu: 1-501-454-1641
Nukushi: 1-501-907-2805
Barua pepe: goats@heifer.org

Special thanks to Peter Mwakabwale and Jim DeVries for translating these pages into Kiswahili.