ADA ZA UANACHA - 2007

Bofya hapa kwa kuomba uanacha mwaka 2007

Uamuzi kuhusu viwango vya ada za uanachama za Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi ulifikiwa wakati wa mkutano wa Bodi uliofanyika mwezi Juni 2006 nchini Romania. Ikiwa kama mkakati wa Umoja wa Wadau wa Mbuzi Kimataifa wa Kuboresha utafiti na maendeleo ya mbuzi duniani kwa manufaa ya binadamu bodi iliamua kupunguza ada ya uanachama kwa watu wanaoishi katika nchi ambazo kiwango chao ni chini ya .500 kulingana na Vielelezo vya umoja wa mataifa vya maendeleo ya Binadamu. Kufahamu zaidi kuhusu Vielelezo vya umoja wa mataifa vya maendeleo ya Binadamu bofya hapa

Maendeleo ya Binadamu ni zaidi ya kupanda au kushuka kwa pato la taifa. Maendeleo ya binadamu yanahusiana na kujenge mazingira ambayo watu watatumia ujuzi walionao kuongeza uzalishaji, kuishi maisha ya ubunifu kulingana na mahitaji na matakwa yao. Watu ndio utajiri halisi wa mataifa. Kwa hiyo maendeleo yanahusu kuwawezesha watu waweze kuwa na uchaguzi wa kuishi maisha wanayo yathamini.~Umoja wa Mataifa

Kulingana na wazo hilo, uamuzi huo wa Bodi utawawezesha watafiti, wazalishaji na maafisa ugani wanaoishi katika nchi hizo kuweza kupata taarifa sahihi na kupanua mtandao wa umoja wa wadau wa mbuzi kimataifa

Vielelezo vya umoja wa mataifa vya maendeleo ya Binadamu (UN-HDI) ni vielelezo mchanganyiko ambavyo vinapima mafanikio katika maeneo makubwa matatu ya maendeleo ya binadamu

  • Maisha marefu na yenye afya (ambayo hupimwa na matarajio ya muda wa mtu wa kuishi)
  • Elimu/maarifa (ambayo hupimwa kwa kuangalia uwezo wa kujua kusoma na kuandika na kiwango cha uandikishwaji wa wanafunzi)
  • Ubora wa maisha ( ambao hupimwa na pato la taifa na mlingano katika uwezo wa kununua bidhaa mbalimbali)

Kuanzia Januari mosi 2007 viwango vya ada za uanachama kwenye Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi utagawanyika katika makundi mawili yaani, kundi la juu na kundi la chini. Wale watakaoomba uanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi ambao wanatoka katika nchi ambazo zipo chini ya .500 kulingana na Vielezo vya umoja wa mataifa vya maendeleo ya Binadamu watawekwa katika kundi la chini. Watu watakaoomba uanacha Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi ambao wanatoka katika nchi ambazo zinaanzia .500 na kuendelea kulingana na Vielezo vya umoja wa mataifa vya maendeleo ya Binadamu watawekwa katika kundi la juu.

Ada za uanchama kwa kundi la chini zitapunguzwa na kufikia

  • Dola za Kimarekani 20 kwa wanachama wa kawaida* ambao pia wanatumia mtandao kupata taarifa za tafiti mbalimbali zinazohusu wanyama wadogo wanaocheua
  • Dola za Kimarekani 60 kwa wanachama ambao watajiandikisha kwa kujaza fomu maalumu pia watapata taarifa za tafiti mbalimbali kupitia mtandao zinazohusu wanyama wadogo wanaocheua

Ada za uanchama kwa kundi la juu zitapandishwa na kufikia

  • Dola za Kimarekani 45 kwa wanachama wa kawaida* ambao pia wanatumia mtandao kupata taarifa za tafiti mbalimbali zinazohusu wanyama wadogo wanaocheua
  • Dola za Kimarekani 145 kwa wanachama ambao watajiandikisha kwa kujaza fomu maalumu* pia watapata taarifa za tafiti mbalimbali zinazohusu wanyama wadogo wanaocheua

*Uanachama wa katika Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi ni pamoja na kupata taarifa mbalimbali kwa mtandao zinazohusu wanyama wadogo wanaocheua kuanzia mwezi Januari na kumalizika mwezi Desemba.

Kwa orodha ya nchi mbalimbali kufuata alfabeti kulingana na viwango vya umoja wa mataifa vya maendeleo ya Binadamu bofya hapa

Kwa orodha ya nchi mbalimbali kulingana na viwango vya umoja wa mataifa vya maendeleo ya Binadamu bofya hapa

Ili kuweza kufidia sehemu ya punguzo hili la ada ya uanachama, kiwango cha ada ya uanachama kwa kundi la juu kimeongezwa kwa dola za kimarekani tano ($5) kutoka katika kiwango chake cha sasa. Hata hivyo ongezeko hili kidogo haliwezi kutosheleza kiwango cha fedha ambacho umoja wa wadau wa mbuzi kimataifa unatarajia kupunguza kwa wanchama wake wa kundi la chini. Kama unafahamu taasisi au shirika lolote ambalo lipo tayari kutusaidia kutoa ruzuku kwa sehemu au kwa ada yote ya uanachama tafadhali tujulishe.

Kwa taarifa zaidi kuhusu Vielelezo vya umoja wa mataifa vya maendeleo ya Binadamu tembelea http://hdr.undp.org/hd/

Au http://en.wikipedia.org/wiki/Human_Development_Index

Bofya hapa kwa kuomba uanacha mwaka 2007

Ukihitaji maelezo zaidi wasiliana na: goats@heifer.org